Ufunuo wa Yohana Mlango 9 Revelation

Ufunuo wa Yohana 9:1 Revelation 9:1

Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.

Ufunuo wa Yohana 9:2 Revelation 9:2

Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.

Ufunuo wa Yohana 9:3 Revelation 9:3

Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.

Ufunuo wa Yohana 9:4 Revelation 9:4

Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.

Ufunuo wa Yohana 9:5 Revelation 9:5

Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu.

Ufunuo wa Yohana 9:6 Revelation 9:6

Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.

Ufunuo wa Yohana 9:7 Revelation 9:7

Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.

Ufunuo wa Yohana 9:8 Revelation 9:8

Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.

Ufunuo wa Yohana 9:9 Revelation 9:9

Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani.

Ufunuo wa Yohana 9:10 Revelation 9:10

Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.

Ufunuo wa Yohana 9:11 Revelation 9:11

Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.

Ufunuo wa Yohana 9:12 Revelation 9:12

Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye.

Ufunuo wa Yohana 9:13 Revelation 9:13

Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,

Ufunuo wa Yohana 9:14 Revelation 9:14

ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.

Ufunuo wa Yohana 9:15 Revelation 9:15

Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

Ufunuo wa Yohana 9:16 Revelation 9:16

Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao.

Ufunuo wa Yohana 9:17 Revelation 9:17

Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.

Ufunuo wa Yohana 9:18 Revelation 9:18

Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.

Ufunuo wa Yohana 9:19 Revelation 9:19

Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo.

Ufunuo wa Yohana 9:20 Revelation 9:20

Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.

Ufunuo wa Yohana 9:21 Revelation 9:21

Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.